Ndege wa ajabu wanaosadikiwa
kutoa kinyesi chenye sumu kali,wamevamia kisiwa cha musira kilichopo Manispaa
ya Bukoba na kusababisha vifo vya mifugo kama ndege anaofugwa,huku ukali wa sumu hiyo
ukisababisha kutoboka mabati ya nyumba zilizopo kisiwani humo.
Ndege hao wanaoaminika kuvamia
kisiwa hicho mwezi mmoja uliopita tayari wamesha sababisha vifo vya kuku 516 na
mbuzi 12 wanaodaiwa kula au kugusa kinyesi chao.Hata hivyo bado haijafahamika
ndege hao wanatokea nchi gani.
Akithibitisha habari hizo mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe anasema serikali ilipata taarifa hizo kupitia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya na baadaye kuundwa timu ya kutafuta taarifa za awali za tatizo hilo.
Massawe alisema pamoja na ndege pamoja na kusababisha vifo vya mifugo na ndege wafugwao pia baadhi ya miti katika kisiwa hicho imekauka na mabati kutoboka inapotokea kinyesi chao kitaangukia kwenye paa za nyumba zao.
No comments:
Post a Comment