Wakati mataifa mbalimbali
duniani yakiadhimisha siku ya Afya ya Figo Duniani leo,ugonjwa huo unaendelea
kuwakumba mamilioni ya watu.Takwimu zinaonyesha kuwa,mwanaume mmoja kati ya
watano,na mwanamke mmojakati ya wanne walio na umri kati ya miaka 65 na 74
wanaugonjwa sugu wa Figo.
*************************
Ndege wa ajabu wanaosadikiwa
kutoa kinyesi chenye sumu kali,wamevamia kisiwa cha musira kilichopo Manispaa ya
Bukoba na kusababisha vifo vya mifugo kama ndege anaofugwa,huku ukali wa sumu hiyo
ukisababisha kutoboka mabati ya nyumba zilizopo kisiwani humo.
**************************
Serikali ya Uchina imechapisha
picha zilizonaswa na mtambo wake wa satelite zikionyesha mabaki ya kitu kipana
kikielea katika bahari ya Kusini mwa Uchina.
Picha hizo zilipigwa siku ya Jumapili, saa ishirini
na nne baada ya ndege ya abiria ya Malaysia kutoweka ikiwa na abiria 239,
lakini haijabainika ikiwa vifaa hivyo ni vya ndege hiyo.
***************************
Rais wa Marekani Barrack Obama, ameonya
Urussi kusitisha mpango wake wa kutaka kutwaa eneo la Crimea nchini Ukraine lasivyo
iwekewe vikwazo.
No comments:
Post a Comment