Pages

Thursday, March 26, 2015

HII NDO DUNIA YETU YA LEO"BABA AWABAKA WATOTO WAKE WADOGO KWA MIAKA MIWILI"


     Rahma Mashamu ambaye ni mama mzazi wa watoto wawili mmoja wa miaka 11 na     mwingine 15 wanaodaiwa kubakwa na baba wa watoto hao akilia kwa uchungu wakati akihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo, wilayani Kibaha mkoani Pwani. Picha na Julieth Ngarabali 

Mkazi mmoja wa Miembe Saba wilayani Kibaha mkoani Pwani amekamatwa na polisi akituhumiwa kuwabaka watoto wake wawili wadogo kwa zaidi ya miaka miwili sasa.


Habari zilizolifikia zilisema kuwa katika tukio hilo ambalo limethibitishwa na polisi na watoto wenyewe, baba huyo alianza kuwafanyia binti zake vitendo hivyo mwaka 2013 kwa siku ambazo mkewe ambaye nimama wa wasichana hao hakuwapo hadi usiku wa Machi 19, mwaka huu.

Kwa sasa tunayahifadhi majina ya familia hiyo.Watoto hao mmoja mwenye umri wa miaka 15 anayesoma darasa la saba na mdogo wake mwenye umri wa miaka 11 aliyeanza kubakwa akiwa darasa la tatu.
Kwa mujibu wa watoto hao, baba huyo alikuwa anamuita mmoja wa watoto wake chumbani kwake na kumtaka alale na mdogo wao wa kiume wakati huo akiwa na mwaka mmoja na binti akipitiwa na usingizi humvua nguo za ndani na kumwingilia huku akimtaka kukaa kimya na kuvumilia maumivu.
Mke wa mtuhumiwa huyo, ambaye amekuwa akizimia mara kwa mara kutokana na kulia baada ya kubaini mchezo huo, alisema aligundua watoto wake wanabakwa Ijumaa iliyopita baada ya mmoja wa mabinti zake hao kumweleza kuwa baba yake alikuwa amembaka Machi 19, mwaka huu.

Alisema kabla ya binti huyo kumweleza hivyo, alimwomba asimpige kwani kuna kitu anataka amweleze, japo ni kibaya lakini yeye amechoshwa na kimekuwa kikimuumiza kichwa.
“Alisema kila ninapokwenda katika biashara zangu, anatamani nisiwe ninawaacha hapo, nikamwahidi sitamfanya kitu ili mradi aseme ukweli tu,” alisema mama huyo.

Baada ya kuhakikishiwa kulindwa, ndipo binti huyo aliposimulia jinsi ambavyo baba yake amekuwa akiwafanyia na kuwatishia wakipiga kelele atawaua.
“Niliposikia mwili ulisisimka na ghafla binti yangu mwingine naye akatokea akilia na kuniambia, ‘hata mimi baba ananifanyiaga hivyohivyo kila siku unapokuwa umepeleka mboga sokoni Kariakoo,” alisema mama huyo.

Mwanamke huyo ameomba sheria ichukue nafasi yake katika tukio hilo kwa kuwa ni la kinyama na pia wataalamu wa saikolojia wamsaidie binti yake mdogo wa darasa la tano kwani yeye ameathirika zaidi.
Daktari aliyewapima watoto hao, ameshauri binti huyo mdogo apate ushauri zaidi ili kurudisha akili yake katika hali ya kawaida.

Wakizungumza nyumbani kwao jana watoto hao, walisema baba yao alikuwa akiwatishia kuwakatakata kwa panga au kuwakaba koo humohumo chumbani endapo wangethubutu kumweleza mtu yeyote kitendo wanachokifanya.
“Tulikuwa tumeingia kwetu kulala na wadogo zangu, nikasikia ananiita nikambembeleze mtoto eti anamsumbua, nilikwenda nikambembeleza  akalala, wakati nashuka kitandani kurudi chumbani kwetu baba akanivuta kwake akanivua, akasema anachokifanya ni suna kwa hiyo hataki kelele, akisikia atanikaba nife.”
“Niliumia sana na asubuhi mama alirudi nikajitahidi kweli asijue na hata shule sikwenda, jioni mama aliondoka tena baba hakuniita siku hiyo lakini baada ya siku tatu aliniita tena ikawa vilevile navumilia. Siku zilivyozidi unaweza kukuta kwa wiki naitwa hata mara nne siku ambazo mama hayupo nyumbani,” alisema.

Watoto hao walieleza kuwa baadaye baba huyo alihamia kwa binti mdogo kwa staili ileile na kila mmoja alikuwa akiitwa kwa zamu na kwa vile kila mmoja alijua ni siri yake na baba. Kutonaka na woga wa kuuawa, hakuna aliyemweleza mwenzake hadi katikati ya mwaka jana mmoja wao alipomweleza mwenzake na baadaye kumweleza mama yao.

“Baba alikuwa anasema atatuua bila hata mtu kujua na tutaozea shambani, hata nikiwa katika siku zangu baba ananiingilia hivyohivyo, naugua kila mara UTI, mdogo wangu naye kila mara UTI, tukaamua liwalo na liwe kama kufa basi ila mama ajue,” alisema mtoto huyo huku akibubujikwa na machozi.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Miembe Saba, Hamis Shomari alisema kabla ya kupelekwa kituo cha polisi Kongowe Jumamosi iliyopita, watoto hao waliitwa shuleni hapo na kuhojiwa kila mmoja peke yake na wote walikiri kuanza kubakwa mwaka 2013 na baba yao na kwamba tabia hiyo iliendelea hadi Machi 19 usiku alipobakwa binti mdogo kwa mara ya mwisho na Machi 20 walipoamua kumweleza mama yao.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alisema wanamshikilia mtuhumiwa huyo na kwamba wasichana hao wamefanyiwa vipimo mbalimbali na majibu ya daktari yamethibitisha kuwa wamebakwa na sehemu zao za siri  zimeharibiwa, hivyo wanaendelea na matibabu.MWANANCHI

No comments:

Post a Comment