Rais Jakaya Kikwete na mwenzake Rais Pierre Nkurunziza wa
Burundi wamezindua safari za treni tatu za mizigo ‘block train’ kutoka Dar es
Salaam kwenda Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Jeshi la Polisi mkoani Simiyu linawashikilia
askari wawili wa magereza na polisi kwa kukutwa na noti bandia ikiwa pamoja na
sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).Kamanda wa Polisi mkoani hapa,
Charles Mkumbo alisema askari hao walikamatwa juzi saa tisa mchana katika Mtaa
wa Old Maswa, Kata ya Nyakabindi, wilayani Bariadi.
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema
kuwazuia wananchi kwenda nyumbani kwake kumshawishi agombee urais katika
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu ni sawa na kuzuia mafuriko kwa mkono.Lowassa
alitoa kauli hiyo nyumbani kwake mjini Dodoma jana wakati alipotembelewa na
kundi jipya kutoka Mbarali mkoani Mbeya waliokwenda kumshawishi atangaze nia
kugombea urais.
Ubalozi wa Marekani nchini Uganda, umesema una
taarifa za uwezekano wa shambulio la kigaidi nchini humo.Aidha Marekani pia
imetoa tahadhari kwa raia wake.Taarifa ya ubalozi huo umebainisha kwamba
shambulio hilo linaweza kutekelezwa wakati wowote, katika maeneo ambayo raia wa
mataifa ya Magharibi na Marekani hukutana.
Saud Arabia imeanza operesheni zake za kijeshi
nchini Yemen, ikiwa ni kujibu ombi la Rais wa nchi hiyo Abd Rabbuh Mansour
Hadi.Balozi wa Saudi Arabia Nchini Marekani amesema kuwa, taifa lake na
washirika wao wa ghuba wanatumia mashambulizi ya angani katika harakati za
kuunga mkono serikali halali ya Yemen, ili isichukuliwe na kundi wa waasi la
Houthi.
Wakaguzi wa kifaransa wamesema wamefanikiwa
kukipata kifaa cha kurekodia sauti na maneno kutoka katika kisanduku cheusi cha
ndege ya shirika la ndege la ujerumani iliyopata ajali katika milima ya Alps.Wakaguzi
hao mpaka sasa wanaendelea kukitafuta kisanduku kingine ,ambacho hurekodi
taarifa za ndege hiyo na chanzo cha ajali hiyo . Timu hiyo ya uokozi iliyoko
katika eneo la ajali lililoko upande wa Kusini mwa Ufaransa wamefanikiwa
kukipata kifaa hicho kinachohifadhiwa katika chumba cha rubani kikiwa
kimeharibika.
No comments:
Post a Comment