Pages

Friday, March 27, 2015

HABARI KWA UFUPI




Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemtaka Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kuripoti haraka Kituo Kikuu cha Polisi,  Dar es Salaam kutoa maelezo kuhusu tuhuma za kashfa na matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.


Wakati wenyeviti wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) pamoja na kamati zake za kitaalamu wanakutana Zanzibar kutafuta suluhu kuhusu mgawanyo nafasi za kugombea katika uchaguzi mkuu ujao, kuna uwezekano mkubwa vyama hivyo kuteua mgombea urais kutoka Chadema.

Raia wa Nigeria kesho wanatarajiwa kujitokeza katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyoHata hivyo kumekuwa na vute ni kuvute huku kuripotiwa taarifa ya Mtendaji Mkuu wa Kampuni inayosambaza mashine za kusoma vitambulisho vya elekroniki vya wapiga kura kukamatwa na maafisa usalama wa nchi hiyo.

Mawaziri 5, makatibu 6 wa kudumu na Magavana 10 wametajwa miongoni mwa maafisa 175 wa umma watakaolazimika kunga'atuka mamlakani katika siku 60 zijazo iliuchunguzi wa kina ufanyike kuhusu madai ya ufisadi dhidi yao.Hayo yalibainika katika ripoti iliyotolewa bungeni na rais Uhuru Kenyatta katika kikao maalum cha bunge la taifa kilichowajumuisha wabunge na maseneta.

Rubani wa ndege ya kampuni ya Germanywings ilioanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa siku ya jumanne alitaka kuiharibu ndege hiyo kulingana na maafisa wa Ufaransa.Kiongozi wa mashtaka katika mji wa Mersaille ,Brice Robin, akizungumza kulingana na habari aliyopata katika kijisanduku cha kunasa sauti katika ndege amesema kuwa rubani huyo alikuwa ndani ya chumba cha kuendesha ndege pekee.

No comments:

Post a Comment