Vitendo vya ubakaji,
kulawiti na wanaume kuanza kufanya mapenzi ya jinsia moja hadi
wanafumaniwa na wake zao vimeshamiri wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro
na sasa uongozi wa halmashauri umelazimika kuingilia kati na kutaka
kuwepo mikakati ya kumaliza tatizo hilo.
Kukithiri kwa vitendo
hivyo kumewekwa wazi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo,
Judathadeus Mboya, wakati wa mkutano ulioandaliwa na Asasi ya Utetezi wa
Haki za Binadamu na Utoaji wa Ushauri wa Kisheria ndani ya Jamii
(AJISO).
“Kumeibuka vitendo vya
watu kufanya mapenzi ya jinsia moja. Kuna matukio ya wanawake kuingia
katika nyumba zao na kuwakuta wanaume wakijihusisha na mapenzi na
wanaume wenzao...ni lazima jamii kuchukua hatua kuhakikisha tabia hiyo
inatokomezwa,” alisema Mboya na kuongeza;
“Vitendo vya ndoa za
jinsia moja yaani mwanaume kufanya mapenzi na mwanaume mwenzake
havikuwepo katika wilaya ya Rombo, lakini leo si vitu vya ajabu, hivi
tumekuwa watu wa lazima tubadilike na kuondokana na aibu hii ambayo ni
mbaya sana,” alisema Mboya.
Mboya, pia alisema kuna
vitendo vya kubakana kulawiti ambapo waathirika wakubwa wa vitendo
hivyo ni watoto. Katika mkutano huo ambao uliandaliwa na AJISO kwa lengo
la kuwatambulisha wasaidizi wa msaada wa kisheria waliopatiwa mafunzo
na shirika hilo, Mkurugenzi huyo alisema kumekuwepo na matukio ya watoto
kulawitiwa na kubakwa.
Alisema hata watoto wa
jinsia moja wamekuwa wakijihusisha na masuala ya mapenzi, huku matukio
hayo yakifanywa kuwa siri. “Hali hii ni udhalilishaji mkubwa katika
jamii,” alisema Mboya na kuongeza kwa kutoa mfano:
“Hivi karibuni katika
eneo la Mamsera wilayani hapa, kuna watoto 10 wa kiume wa shule za
msingi, ambao walikuwa wanachezeana mchezo mchafu (kulawitiana) na mtoto
mmoja ambaye alikuwa mdogo zaidi, aliathirika vibaya sana na taarifa
zilifika ofisini na watoto wale walikamatwa, lakini yule aliyekuwa
mkubwa aliyehusika kuwaumiza wenzake alikimbia na hadi sasa anatafutwa
na polisi, hili ni jambo la hatari na aibu.”
Alisema, halmashauri
hiyo pia itatoa elimu kwa jamii kwa njia mbalimbali ikiwemo mikutano ya
hadhara, ili kuwapa uelewa na kuwawezesha kutoa taarifa za matukio ya
ulawiti na ubakaji, hatua ambayo itasaidia kutokomeza vitendo hivyo
katika wilaya hiyo.
Alisema Halmashauri
hiyo pia itatoa elimu kwa jamii kwa njia mbalimbali ikiwemo mikutano ya
hadhara, ili kuwapa uelewa na kuwawezesha kutoa taarifa za matukio ya
ulawiti na ubakaji, hatua ambayo itasaidia kutokomeza vitendo hivyo
katika wilaya hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na AJISO katika kipindi cha mwaka jana 2013 kulikuwa na
matukio 115 ya ubakaji na kulawiti yaliyoripotiwa katika shirika hilo.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Anthony Tesha, alisema jani linaloitwa
isale limekuwa likitumika kuombea msamaha kwa kabila la Wachaga,
limekuwa likitumika vibaya kwa baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo, na
kuchangia kuongezeka kwa vitendo vya kikatili na udhalilishaji kwa
watoto na wanawake.
Tesha alisema jani hilo
la isale ambalo ni vigumu kulikosa kwenye shamba la watu wa kabila la
Kichaga, limekuwa likitumika katika maeneo mengi ya wilaya hiyo kufunika
maovu, kutokana na kutumika kwenda kuombea msamaha pindi panapotokea
mtu kujihusisha na vitendo viovu ikiwemo ubakaji na ulawiti kwa watoto,
hivyo kuwa kichocheo kikubwa cha kuendelea kwa vitendo hivyo katika
jamii.
“Mtoto anabakwa au
analawitiwa Rombo, mzazi unaletewa Sale unafunika uovu ule na kupoteza
ushahidi kabisa, hii ni hatari sana katika jamii, kwani vitendo hivi
bado vimeen delea kushika kasi katika wilaya hii na waathirika wakubwa
ni watoto wetu ambao ndio wanategemewa kuja kulijenga taifa hili hapo
baadaye,” alisema Tesha.Chanzo Majira
No comments:
Post a Comment