Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch
linasema kuwa zaidi ya raia 2,000 wameuawa nchini Nigeria mwaka huu na
wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Kwa mujibu wa shirika hilo, vifo hivyo vimetokea
katika mashambulizi 95 tofauti katika zaidi ya miji 70 na vijiji
kaskazini mashariki mwa taifa hilo.
Rais Goodluck Johnathan amepata shinikizo la
kusitisha mashambulizi hayo na kuwaokoa zaidi ya wasichana 200 wa shule
waliotekwa nyara miezi mitatu iliopita.
Anatarajiwa kukutana na baadhi ya familia za
wasichana hao kufuatia ombi la mwanaharakati wa Pakistan Malala
Yousafzai ambaye alikutana naye hapo jana.BBC
No comments:
Post a Comment