Pages

Tuesday, July 15, 2014

HABARI KWA UFUPI



Vitendo vya ubakaji, kulawiti na wanaume kuanza kufanya mapenzi ya jinsia moja hadi wanafumaniwa na wake zao vimeshamiri wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro na sasa uongozi wa halmashauri umelazimika kuingilia kati na kutaka kuwepo mikakati ya kumaliza tatizo hilo.

Mbunge wa Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, David Kafulila, amesema haogopi kushtakiwa na kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited ( IPTL) kwani hata watu wasio na haki wana ujasiri wa kwenda mahakamani.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameingia matatani baada ya Mahakama ya Wilaya ya Hai kuona ana kesi ya kujibu katika mashtaka ya kumshambulia mwangalizi wa ndani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) imetoa tamko zito ikieleza kushangazwa na kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kupinga mapendekezo yaliyomo katika Rasimu ya Katiba iliyotokana na maoni ya Watanzania na kusema kitendo hicho kimeishusha hadhi Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyoiteua.

Israel na Kundi la Hamas nchini Palestina zimesema , zitazingatia mapendekeo ya kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza yaliyotolewa na Misri.Chini ya mpango huo , makubaliano ya kusitisha vurugu hizo zilizodumu takriban wiki moja yatatekelezwa mapema hivi leo Jumanne.

Stand United, ambayo imepanda Ligi Kuu msimu ujao imekivunja kikosi cha Toto Afrika baada ya kuwasajili wachezaji wawili wa timu hiyo, Kheri Mohamedi na beki kisiki John Bosco, huku wengine wengi wakiwa njiani kuelekea katika timu hiyo.

No comments:

Post a Comment