Pages

Sunday, July 13, 2014

KWA WALE WAJASIRIAMALI KARIBUNI VIFARANGA VYA KUKU WA NYAMA AMBAYE PIA KUKU HUYO HUYO HUTAGA MAYAI

Kuku huyu ni wa nyama na pia anataga mayai ambayo yanauwezo wa kutotoa vifaranga ila yeye hana uwezo wa kulalia mayai,hivyo ukipata mayai unaweza kumuwekea kuku mwingine wa kienyeji alalie na baada ya siku 21 utapata vifaranga wako.Kuku huyu anauzito wa kilo 3 hadi 5 kulingana na utakavyompa chakula chenye virutubisho na kuhusu ukuaji wake hadi kufikia kutaga Mayai ni miezi mitano hadi sita.

Namshukuru Mungu niliweka mayai kwenye mashine yangu tarehe 22/06/2014 na kuanzia jana nimeanza kutoa Vifaranga,karibuni Wajasiriamali wenzangu tuungane mkono.
Hawa ndiyo vifaranga wa kuku uliyemuona hapo juu,kifaranga kimoja nauza Sh 2,000 kama unachukua  vifaranga kuanzia 50 kwenda juu ni Sh 1,800 kwa kifaranga.KARIBUNI SANA WAJASIRIAMALI WENZANGU.

No comments:

Post a Comment