Halmashauri
ya Wilaya ya Ngorongoro imeanza kutekeleza kazi ya kutoa chanjo dhidi ya
magonjwa yanayozuilika kwa watoto zaidi 5,000 wa jamii ya wafugaji wa Kimasai
wanaoishi katika kata saba za Tarafa ya Ngorongoro zilizoko ndani ya eneo la
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCCA).
Polisi
mkoani Kigoma wamelazimika kutumia risasi za moto kuwatawanya watu waliokuwa
wakifanya vurugu kwa kuchoma nyumba mbili za watu kwa tuhuma za ushirikina.
Mamia
ya Wapalestina wamekuwa wakikimbia sehemu za kaskazini za Gaza, baada ya Israel
kuonya kuwa italenga sehemu hiyo katika mashambulio yake ya sasa.Umoja wa
Mataifa umenukuliwa ukisema kuwa watu kama 4,000 tayari wameomba hifadhi katika
hifadhi ya muda.
Wachimba
migodi wa Afrika Kusini wamekataa nyongeza ya mishahara iliyopendekezwa na
makampuni ya migodi.Chama cha wachimba migodi, NUMSA, chama kikubwa kabisa cha
wafanyakazi Afrika Kusini,
Maafisa
wa Palestina wanasema kuwa watu kumi na saba wa familia moja wameuawa baada ya
makombora ya Israel kuharibu nyumba moja ya ghorofa tatu ya mkuu wa polisi wa
Hamas.Tayseer Al-Batsh anadaiwa kujeruhiwa katika shambulizi hilo.
No comments:
Post a Comment