Pages

Thursday, July 24, 2014

HABARI KWA UFUPI



Watuhumiwa sita wa matukio ya ugaidi katika Jiji la Arusha jana walipandishwa kizimbani wakiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi kujibu tuhuma za kufanya matendo ya kigaidi.


Watu wapatao 40, wameuawa katika milipuko mikubwa miwili iliyotokea katika mji wa Kaduna, kaskazini mwa Nigeria. Katika mlipuko wa kwanza wa kujitoa mhanga watu 25 waliuawa, huku wengine 15 wakiuawa katika eneo lililokuwa na msongamano wa watu katika mji wa Kawo.

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Temple, Marekani wamegundua dawa ya kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) ambayo ni ya uhakika zaidi ukilinganisha na zilizowahi kupatikana katika tafiti za awali duniani.Dawa yao inaweza kutumika kwa tiba ya wanaoishi na VVU na kinga kwa wale ambao bado hawajaambukizwa.

Madaktari nchini India wametumia saa 7 kufanikisha upasuaji wa kinywa cha kijana Ashik Gavai mwenye umri wa miaka 17 aliyekuwa akipata maumivu ndani ya kinywa.Dr Sunanda Dhiware, mkuu wa Kitengo cha tiba ya meno katika hospitali ya JJ mjini Mumbai ameiambia BBC kuwa wamefanikiwa kuyang’oa meno 232 kinywani mwa Ashik aliyeletwa hospitalini hapo akiwa amevimba taya huku akilalamika kwa maumivu makali.

Ndege ya Abiria ya Kampuni ya Trans Asia ya Taiwan imedondoka wakati ikijaribu kutua kwa dharura na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.Waziri wa usafiri wa Taiwan Yeh Kuang-Shih amesema watu 47 wamefariki na 11 kujeruhiwa katika ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria 54 na wafanyakazi wa ndege wanne.

No comments:

Post a Comment