Ndege ya Abiria ya Kampuni ya Trans Asia ya Taiwan imedondoka wakati
ikijaribu kutua kwa dharura na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.
Waziri
wa usafiri wa Taiwan Yeh Kuang-Shih amesema watu 47 wamefariki na 11
kujeruhiwa katika ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria 54 na wafanyakazi
wa ndege wanne.
ATR 72 iliondoka Kaohsiung lakini ikapoteza
mawasiliano baada ya mwendo wa saa moja ndipo ikaanguka na na kunawaka
moto katika kijiji cha xixi kisiwani Penghu.
Meneja Mkuu wa
TransAsia Hsu Yi-Tsung huku akilia, ameomba msamaha kwa ajali hiyo na
akaahidi kuongeza juhudi za uokoaji na pia kuwasafirisha ndugu wa
waliopoteza maisha kwenda kwenye eneo la tukio.
Siku za hivi karibuni
Taiwan imepigwa na upepo mkali uliombatana na Mvua zilizoletwa na
kimbunga Matmo, hata hivyo wanaosimamia anga katika eneo hilo wamesema
hali ya hewa iliyokuwepo muda huo haikuwa inazidi kiwango kinachoweza
kuzuia ndege kutua.
Habari za kuanguka kwa ndege hii kunakuja wakati
visanduku viwili vya kutunzia kumbukumbu ya ndege ya malaysia iliyoangua
nchini Ukraine tarehe 17 mwezi huu vikiwa vimefika mikononi mwa
wataalamu wa masuala ya anga ili kuchunguza ni ni kitu gani kiliisibu
ndege hiyo.BBC
No comments:
Post a Comment