Pages

Thursday, June 05, 2014

HABARI KWA UFUPI



Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof. Juma Kapuya (CCM), ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi wa zamani, jana alijikuta katika wakati mgumu wa kuumbuliwa na mbunge mwenzake wa Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), wakati wawili hao wakibishania uuzwaji tata wa Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA).


Bunge limeishauri serikali kupitia upya mikataba ya gesi na kampuni za nje ili kubaini kama kweli maslahi ya taifa yamezingatiwa.Ushauri huo ulitolewa jana bungeni na Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara wakati Mwenyekiti wake, Luhaga Mpina, akisoma utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Fedha na Uchumi pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2014/2015.

Baba mzazi wa mwanafunzi wa kidato cha tatu Sekondari ya Mwanza, Annastazia Magafu, Luckford, ambaye anadaiwa kumchoma moto mtoto wake na kumsababisha kifo ameachiwa huru ili kupisha uchunguzi wa kisayansi.

Kiwango cha nauli kitakacholipwa baada ya kukamilika kwa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) kinaelezwa kuwa ni kidogo ukilinganisha na kile kinacholipwa na abiria sasa.

Maafisa nchini Syria wamesema kuwa Bashar Al Assad amechaguliwa tena kama rais wa nchi hiyo.Assad amepata asili mia 89 ya kura zote. Uchaguzi huo umefanyika katika mazingira ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na inaaminika kuwa raia waliokuwa katika maeneo yanayoshikiliwa na serikali pekee ndio waliofanikiwa kupiga kura.

Viongozi wa mataifa tajiri ya magharibi wanaokutana mjini Brussels wamesema kuwa wako tayari kuweka vikwazo zaidi kwa Urusi iwapo itaendelea kuvuruga amani mashariki mwa Ukrain.

No comments:

Post a Comment