Pages

Thursday, June 26, 2014

HABARI KWA UFUPI



Watu sita kati ya 12 wanaotuhumiwa kwa uchochezi na kuvunja chumba cha kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya Kaigara wilayani hapa, jana wamepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya mahakama.


Majambazi wawili jana walizua taharuki katika Mji wa Geita baada ya kuvamia na kupora fedha katika maeneo mawili tofauti kisha kumuua mtoa huduma za fedha kupitia mitandao ya simu.Katika tukio la kwanza juzi saa 11.38 jioni, majambazi hao walivamia duka la Kampuni ya Blue Coast Investment inayosambaza bia mjini hapa na kupora zaidi ya Sh1 milioni.

Taarifa kutoka Somalia zinasema kwamba kumekuwa na makabiliano makali milipuko na milio ya risasi ikisikika katika eneo la hoteli moja inayotumika kama makao makuu ya vikosi vya Afrika vya kulinda amani.Walioshuhudia shambulizi hilo wanasema hoteli hiyo iliyopo katika mji wa Bulo- burde, umeshambuliwa na wanamgambo wa Al -shabaab.

Kumetokea shambulizi la bomu mbele ya soko lenye shughuli nyingi katika mji mkuu wa Nigeria Abuja na kuwauwa zaidi ya watu 21.Taswira ya majonzi na kilio ilitanda katika mji wa Abuja, mamia ya watu waliokuwa wakinunua bidhaa katika soko hilo wakijikuta wakivuja damu kutokana na majeraha ya mlipuko huo na wengine kuishia mauti.

Polisi nchini kenya wamemtia mbaroni gavana wa jimbo la Lamu lililokumbwa na mapigano hivi majuzi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 65.Polisi walimshika Issa Timamy,kufuatia tuhuma za kuhusika na mashambulizi yaliyotokea Mpeketoni mapema mwezi huu.

No comments:

Post a Comment