Takriban watu kumi wameuawa
katika shambulizi la kijiji kimoja kazkazini mashariki mwa
Nigeria,karibu na eneo ambalo zaidi ya vijana 200 walitekwanyara mnamo
mwezi Aprili.
Wakaazi wanasema kuwa watu waliojihami walivamia
kijiji cha Korongi-nim kilichopo takriban kilomita 14 kutoka Chibok
ambapo wasichana hao walitekwa nyara na wapiganaji wa Boko Haram.
Kiongozi moja wa eneo hilo ameiambia BBC kwamba wanamgambo hao walikichoma kijiji chote cha Koronginim.
Ripoti pia zinaarifu kuwa kundi hilo limedaiwa
kuwatekanyara wanaume na wasichana kutoka kijiji chengine katika jimbo
la Yaza siku ya alhamisi.
No comments:
Post a Comment