Msemaji wa kundi la weusi Nikki
wa pili amesema wamefurahia ushindi wa Fid Q kwa sababu wanamkubali kuwa ni
mwanamuziki makini anayejitahidi katika utunzi wa rap.
Alisema tuzo za Kilimanjaro Music
Awards(KTMA)kwa mwaka huu,zimeamsha ari mpya kwa wasanii kutokana na haki
iliyotendeka kwa kuuchagua muziki mzuri kutwaa tuzo.
“Weusi tumeufurahiwa ushindi wa
Fid Q tunaamini ataendelea kufanya vizuri ili kuendesha gurudumu la muziki wa
hiphop mbele huku akitoa msaada kwa chipukizi wa muziki huu.”alisema Nikki wa
pili
Akizungumzia tuzo za Weusi, rapa
huyo alisema wamefurahi kupata tuzo mbili,ikiwemo kikundi bora cha muziki wa
kizazi kipya na wimbo bora wa Hiphop kutokana na wimbo wao wa “Nje ya Box” .
No comments:
Post a Comment