Dodoma. Bunge la Bajeti linaanza leo mjini Dodoma huku wabunge
wakitarajiwa kuanza kulipwa viwango vipya vya posho, ambazo ni Sh300,000
kwa siku sawa na kiwango wanacholipwa wajumbe wa Bunge Maalumu la
Katiba.
Kabla ya kufikia uamuzi wa kupandisha viwango hivyo kwa Sh100,000 zaidi, wabunge walikuwa wakilipwa Sh200,000 kwa siku (yaani Sh70,000 kama posho ya kikao (sitting allowance), Sh80,000 posho ya kujikimu (perdiem) na Sh50,000 ya gharama za usafiri).
Nyongeza hiyo kwa kila mbunge kwa siku, sawa na asilimia 50, italigharimu Bunge la Jamhuri ya Muungano kiasi cha Sh18.5 bilioni kwa siku 52 zilizotengwa kwa ajili ya Bunge la bajeti linalotarajiwa kuhitimishwa Juni 27.
Januari mwaka 2012, Rais Jakaya Kikwete alikataa maombi ya Bunge ya kutaka nyongeza ya posho ipande hadi Sh330,000 na badala yake wabunge hao wakapata nyongeza ya Sh50,000 tu kwa ajili ya usafiri.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililla alipoulizwa kuhusu nyongeza hiyo, hakuthibitisha wala kukanusha, lakini akafafanua kwamba hilo ni suala la uongozi wa Bunge na si la kiutendaji.UDAKU
No comments:
Post a Comment