Pages

Thursday, May 01, 2014

VURUGU ZATOKEA ETHIOPIA BAADHI WAUAWA


                                         Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn

Habari zinasema kumetokea vurugu za wanafunzi katika miji mbali mbali katika eneo la Oromia nchini Ethiopia.


Wakazi wa eneo la Ambo wanasema maafisa usalama walifytua risasi kwa wanafunzi ambazo zimewaua na kuwajeruhi baadhi yao."Wakazi wa eneo la Ambo wanasema maafisa usalama walifytua risasi kwa wanafunzi ambazo zimewaua na kuwajeruhi baadhi yao."
Ofisi ya Mambao ya Nje ya Uingereza imesema kumekuwa na hali vurugu na wasi wasi katika eneo la Ambo siku ya Jumatano.

Watu wa jamii ya Oromo hivi karibuni walikuwa wakipinga mpango kupanua mji mkuu wa Adis Ababa ambao wanasema waingilia mipaka yao.

Serikali ya Ethiopia katika siku za hivi karibuni walitia mbaroni waandishi wa habari na wafuasi wa chama kimoja cha upinzani.BBC

No comments:

Post a Comment