Naibu Spika wa
Bunge, Job Ndugai amenusurika kujeruhiwa na kundi la vijana waliokuwa wakipinga
ongezeko la ushuru wa mazao na kuvamia ukumbi wa mkutano wa Kilimo uliopo
Kibaigwa, wilayani Kongwa.Katika vurugu hizo, ambazo zililazimisha polisi kurusha
mabomu ya machozi ili kuwatawanya waandamanaji, pia mali mbalimbali
ziliharibiwa, likiwemo gari la Mbunge wa Tanga Mjini, Omary Nundu.
Mahabusu wa Gereza
Kuu la Mkoa wa Arusha, jana walizua tafrani katika viwanja vya Mahakama ya
Hakimu Mkazi jijini hapa, baada ya kuvua nguo na kugoma kushuka kwenye basi
wakipinga kitendo cha watuhumiwa wawili wa dawa za kulevya kuachiwa kinyemela.Watuhumiwa
wanaolalamikiwa ambao mashtaka yao yalibadilishwa mara mbili ili wapewe dhamana
ni Dharam Patel (26) na Nivan Patel (20) wanaodaiwa kukamatwa na kete 173 za
heroini na misokoto 300 ya bangi, Aprili mwaka huu.
Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba amesema
wajumbe wa kundi la walio wengi linaloundwa na wabunge wa CCM na baadhi ya 201
katika Bunge la Katiba hawawezi kupitisha Katiba kwa kuwa hakuna maridhiano.
Marekani
imetangaza kwamba imetuma kikosi cha wataalamu nchini Nigeria kusaidia
kuwatafuta wasichana takriban 200 wa shule waliotekwa nyara mwezi uliopita na
wapiganaji wa kundi la Boko Haram.Rais Barack Obama ameshutumu utekaji nyara wa
wasichana hao na kusema kuwa mataifa yanapaswa kufanya kazi kwa pamoja ili
kulikomesha Boko Haram.
No comments:
Post a Comment