Pages

Friday, May 02, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI



Maadhimisho ya sherehe za Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ambayo kitaifa yalifanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana, yameingia dosari baada ya ofisa wa Ikulu, Rashid John Chilwangwe kufariki dunia akiwa katika maadhimisho hayo.


Mauaji ya kikatili yameibuka tena mkoani Geita baada ya watu wasiojulikana kuvamia maeneo matatu usiku wa Aprili 27 na kuwaua kwa kuwachinja na kutenganisha viungo vyao watu watatu kwa imani za kishirikina.Tukio la kwanza la mauaji hayo limetokea katika Kitongoji cha Chemamba, Kijiji cha Chikobe, Kata ya Nyachiluluma ambapo Joyce Matalama (70) alichinjwa na kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiofahamika.

Maafisa nchini Nigeria wanasema kuwa watu 19 wameuawa baada ya mlipuko kutokea katika kituo cha basi katika mji mkuu wa taifa hilo Abuja.Kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya kushughulikia mikasa na hali ya dharura- FEMA- Abbas G Idriss, watu 60 walijeruhiwa vibaya lakini sitaka kati yao wametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Amesema kuwa magari sita yameharibiwa katika mlipuko huo.

Maafisa nchini Colombia bado wanajaribu kuwanusuru takriban watu thelathini waliozikwa wakiwa hai na mamia ya tani ya tope pamoja na mawe baada ya mgodi haramu wa dhahabu kuporomoka usiku wa jumatano.Miili mitatu imepatikana lakini maafisa wanasema kuwa udongo uliolewa chepechepe katika eneo hilo umefanya juhudi za uokoaji kuwa ngumu .


No comments:

Post a Comment