Siku moja baada ya mmoja kati mawaziri wanaotajwa kuwa
mizigo, Christopher Chiza, kupata wakati mgumu kupitisha bajeti ya wizara yake
ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoundwa na
wabunge wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),
imepania kukwamisha
bajeti ya Wizara ya Maji, inayoongozwa na waziri mwingine mzigo, Profesa
Jumanne Maghembe.
Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania (TPSF) imehamasisha jumuiya ya wafanyabiashara nchini
kuchangamkia fursa za biashara katika Umoja wa Mataifa (UN).Wito huo ulitolewa
na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, katika semina ya kuwahamasisha
wafanyabiashara wa Tanzania kufahamu na kuzitumia fursa za biashara
zinazojitokeza UN.
Serikali imekiri
kupoteza mabilioni ya fedha kila mwaka ambazo zinapaswa kulipwa kwa
mujibu wa sheria na makampuni ya migodi nchini kama ushuru wa
huduma kwa halmashauri zinazozunguka migodi hiyo.Naibu Waziri wa Nishati
na Madini, Stephen Masele, alieleza hayo mwishoni mwa wiki wakati alipozungumza
na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Tarime, mkoani Mara baada ya kukabidhi
hundi ya dola 800,000 za Marekani (sh bilioni 1.3) ambazo zimetolewa na mgodi
wa North Mara kama deni la mrahaba kwa Halmashauri ya Tarime.
Chama cha Waganga
wa Tiba Asili Nchini (ATME), Mei 15, mwaka huu kinatarajia kukutana na wahariri
40 kutoka vyombo mbalimbali vya habari kwa ajili ya kuwapa semina juu ya huduma
ya tiba hiyo.Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana,
Mratibu wa ATME Taifa, Boniventure Mwalongo, alisema wameamua kukutana na
wanataaluma hao kama njia mojawapo ya kufikisha yale yote muhimu yanayohusu
afya na tiba asili, ili hatimaye yaweze kuwafikia wananchi.
Saa
chache tu baada ya kutiwa saini kwa mkataba wa usitishaji mapigano nchini Sudan
kusini Malumbano yameibuka .Sasa Serikali na wapiganaji wa Sudan Kusini
wanalaumiana kila upande ukimshutumu mwenzake kuvunja makubaliano hayo
yaliyosainiwa ijumaa.Hata hivyo kiongozi wa waasi Riek Machar anasema bado
ameazimia kutekeleza makubaliano hayo licha ya kwamba anasema serikali ya rais
Salva Kiir inavunja mapatano hayo.
Kiongozi
wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru
wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na
serikali ya Nigeria wataachiliwa huru.Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi
hilo, kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika
kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.
No comments:
Post a Comment