Rais wa korea kusini Park Geune-hye akitoa rambirambi
zake kwa mmoja wa wazazi wa wanafunzi waliokufa kwenye
meli iliyozama mwezi uliopita.
zake kwa mmoja wa wazazi wa wanafunzi waliokufa kwenye
meli iliyozama mwezi uliopita.
Nahodha na wafanyakazi wengine watatu wa feri
iliyozama katika ufuo wa Bahari Korea Kusini mwezi uliopita wameshtakiwa
kwa kosa la kuua bila kukusudia.
Wanashtakiwa kwa kuondoka kwenye feri hiyo, ijulikanayo kama Sewol, huku wakiwambia abiria wao kuwa wasiondoke chomboni.
Wafanyakazi wengine 11 wa meli hiyo wanakabiliwa na mashtaka ya kuzembea kazini.
Zaidi ya abiria 280 - wengi wao wakiwa wanafunzi wa shule ya upili karibu na Seoul - walikufa maji wakati feri hiyo ilipozama.BBC
No comments:
Post a Comment