Mtoto Nasra Rashid (4) aliyefichwa katika boksi kwa miaka minne
mkoani Morogoro, sasa anaopumulia mashine katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili
Nasra, alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,
alipohamishiwa Mei 26 mwaka huu kwa ajili ya uchunguzi zaidi akitokea
katika Hospitali ya mkoa wa Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Daktari
bingwa wa Magonjwa ya Watoto, David Kombo, aliyekuwa zamu alisema
Nasra, aliwekewa mashine maalum ili kusaidia kupata hewa ya Oksijeni
baada ya kuanza kupumua kwa shida.
Alibainisha kuwa hali ya mtoto huyo ilikuwa ikiendelea vizuri lakini
juzi usiku ilibadilika na hivyo kuwekewa mashine ya kupumulia.
Dk. Kombo alisema kutokana na hali hiyo, madaktari wa zamu juzi
waliamua kumfanyia vipimo na kubaini anasumbuliwa na Ugonjwa wa Nemonia.
Dk. Kombo, alisema mtoto huyo akipata nafuu ya ugonjwa wa Nemonia,
ataendelea na vipimo vikubwa vya mwili mzima ikiwamo moyo na figo.
Alisema licha ya ya kumpatia dawa za Nemonia, wanaendelea kumpatia
chakula na dawa baada ya vipimo vya awali kubaini ana Utapiamlo.
Ofisa Muuguzi wa zamu, Iluminata Sokani, alisema licha ya kupumulia
mashine hali ya mtoto huyo inaendelea kuimarika kila wanapomfanyia
vipimo kujua maendeleo yake.
Naye mama mlezi wa Nasra, Josephine Joel alisema kabla ya mtoto
hajawekewa mashine ya kumsaidia kupumua, alimuambia anaumia kifuani na
kiunoni
Mtoto Nasra alifichuliwa na Mei 2, mwaka huu na majirani ambao
walimweleza Ofisa Mtendaji wa Kata ya
Kiwanja cha Ndege Dia Zongo kuwa
alikuwa amefichwa katika boksi na Mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la
Mariamu Said mkazi wa Kata hiyo mkoani Morogoro.
Majirani hao walimweleza Zongo kuwa Nasra alifichwa ndani ya boksi
tangu akiwa na umri wa miezi tisa 2009 na kwamba hafanyiwi usafi wala
kumtoa nje.TANZANIA DAIMA
No comments:
Post a Comment