Kama kuna yeyote anayehisi kwamba
Beyonce na Jay Z hawako sawa si sahihi,watu hawa mwanzoni mwa wiki hii
walifanyiana tukio lililovutia sana.
Wakati Beyonce akipita kwenye
zulia jekundu katika hafla ya Mett Ball 2014 iliyofanyika kwenye nyumba ya
sanaa ya Metropolitan Jumatatu mjini new York,alipoteza pete yake ampapo
ilianguka pasipo kujua.
Katika tukio hilo Jay Z aliiona
pete hiyo hivyo kwa haraka akaenda kuichukua na kurudi kwenye zulia jekundu
ambapo Beyonce alikuwa akipita,kilichotokea alipiga magoti kama mwanaume
anayeomba uchumba kwa mwanamke na kumvalisha.
No comments:
Post a Comment