Kibongo bongo hii ni furaha kubwa sana maana wazee wengi hukataa uzee na hata ukiwasalimia hawasiti kukwambia kuwa unanisalimia unataka kuninyima nini,au wengine hujibu nimekuzalia wazazi wako.Hiyo imepelekea kuibuka maneno mengi ya hapa na pale ikiwemo ya kusema uzee mwisho Chalinze.
Vyuo vikuu vitatu maarufu duniani
vimekuja na matokeo ya utafiti ambao hawatamani kamwe kuzeeka.Utafiti wa vyuo
vya Harvard na California vya nchini Marekani vikishirikiana na Cambridge
nchini Uingereza,unajenga mazingira ya kuifanya ndoto ya wenye mawazo ya
kuukataa uzee kuwa kweli.
Watafiti hao wilichukua damu ya
panya mchanga nakumuingizia kwa aliyezeeka,walichobaini ni kwamba Panya Yule mzee
alichangamka na kurejewa na nguvu za ujana.
Matokeo yautafiti huo yanatoa
mwanya kwa wanasayansi kukaa kitako na kutengeneza dawa ambayo mtu akitumia anaweza
kutozeeka.
Kutozeeka huko ni kuendelea kuwa
na dalili za ujana kama vile kutokuwa na makunyanzi usoni na viungo kuendelea
kuwa na nguvu ya kutekeleza mambo yote kama kawaida hata wenye umri wa zaidi ya
miaka 70.
Nini kinasababisha
uzee.
Wataalamu wanasema kuwa ni jambo
ambalo liko wazi kwamba uzee unapozidi mwili hushidwa kujimudu na hatimaye
kusababisha kifo.
Utafiti uliosimamiwa na mtaalamuwa
Elimu ya Viumbe katika Chuo kikuu cha Michigan nchini Marekani,Dk John Langmore
ulibaini kuwa mtu anakufa kwa umri kutokana na viungo vya mwili kushindwa
kutekeleza kazi zake kikamilifu.
Hali hiyo inachangiwa na kasi ya
seli za mwili kuzaliana kupungua kwa kiwango kilichopindukia huku zinakufa zikiwa
nyingi.Mfumo huo uko hivi,mtoto anapozaliwa ukuaji wake ni wa kasi sana.Hii
inatokana na uwiano wa seli zinazokufa kuwa kidogo zaidi ukilinganisha na zile
zinazozalishwa.
Uwiano wa seli zinazokufa na
zinazozalishwa hufikia mahali ukalingana.Ikifikia kiwango hicho mtu huwa hakui
tena.
No comments:
Post a Comment