Pages

Friday, April 18, 2014

WEMA AMFUNGIA DIAMOND....ASHINDWA KUMZIKA GURUMO



Haya yanawezakuwa mambo ya maloveeeee! Kuna madai kwamba Nasib Abdul Diamond alishindwa kushiriki zoezi la la kuuaga mwili wa mwanamuziki mkongwe Tanzania,marehemu Muhidini Gurumo kwa sababu alifungiwa asitoke ndani na mwandani wake Madam Wema Sepetu Ijumaa linakudadavulia.
Imedaiwa kuwa Wema alimfanyia umafia mpenzi wake huyo April 15,mwaka huu ambapo ilikuwa ndiyo siku ya mwili huo kuagwa nyumbani kwake Mabibo Jijini Dar na kwenda kuzikwa kijijini Masaki,Kisarawe Pwani.
Itakumbukwa kuwa Diamond ndiye msanii aliyewahi kumpa zawadi ya Gari Marehemu Gurumo kutokana na kuguswa na mchango wake katika tansia ya muziki nchini.
Kwa mujibu wa mashuhuda ,wa kitendo cha Diamond kutoonekana katika mazishi hayo ni kama amejishushia heshimakubwa aliyojijengea pale alipomthamini marehemu huyo kwa kumpa Gari aina ya Toyota Funcargo.
“Tulitegemea tungemwonamsibani lakini lakini kwa kutokuwepo kwake ni kama mchango wake wa kumpa Gari Gurumo hauna maana “alisema shuhuda aliyekuwepomsibani
Mapaparazi wetu walidamka asubuhi hadi nyumbani kwa marehemu Gurumo na kujumuika na waombolezaji.
Baada ya mapaparazi wetu kufanya upekuzi yakinifu msibani hapo,walibaini kuwa Diamond hakutia ‘maguu’ hivyo shuguli ya kumsaka ikaanza.
Breki ya kwanza ikawa kwa mapaparazi wetu ilikuwanyumbani kwa Diamond Sinza-Mori jijini Dar ambako hawakumkuta.
Mapaparazi hawakuchoka wakahamishia majeshi nyumbani kwa mwandani wake Wema,Makumbusho Dar ambako mlinzi alibainisha kuwa Diamond yupo na ‘bebi’ wake Wema.
Mapaparazi waliondoka na kurudi tena saa 8:37 mchana ambapo pia waliambiwa wapendanao hao bado wamejifungia ndani,wakaondoka hadi muda wa  jioni baada ya shuguli za mazishi,wakarejea tena na kuambiwa Diamond alitoka muda si mrefu pasipo kujulikana alikoelekea.
Waandishi wetu walimvutia waya Diamond lakini simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Kusaka data zaidi,mapaparazi wetu walimtafuta meneja wa msanii huyo,Babu Tale ambaye alidai kuwa eti Diamond alikuwepo msibani Mabibo lakini hakwenda kisarawe ambako mazishi yalifanyika.
“Tulikuwepo nyumbani kwa marehemu.Nnilikuwa mimi na Diamond tena tumefikamuda huo huo ndiyo mwili ukawa unapelekwa kwenye gari.
Huwezi amini tulijumuika kuupandisha kwenye gari na sisi tukarudi nyumbani kuendelea na shuguli zetu“alisema Babu Tale
Mapaparazi wetu baada ya kutoshibishwa na maelezo hayo,juzi juzi jumatano walimtwangia simu Diamond ambaye alizungumza kwa kujikanyaga.”Mh nilikuwepo msibani lakini sikwenda kuzika tu maana nilikuwa n Babu Tale pale na tulikuwa karibu na gari la Global Publishers,mara tu baada ya kumaliza kuupandisha mwili wa marehemu kwenye gari tuliondoka na kurejea kwenye majukumu yetu “alisema Diamond
Mapaparazi wetu walikuwa jirani na Gari alilotaja Diamond lakini hawakumuona staa huyo achilia mbali waombolezaji wengine ambao waliuliza kwanini msanii huyo hakufika kwenye msiba wa rafiki yake mkubwa!

No comments:

Post a Comment