Rais Jakaya Kikwete amekemea vitendo vya wajumbe wa Bunge la Katiba kuwatusi
waasisi wa taifa hili na kusema huo ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa adabu.Katika
mazungumzo yake na wahariri wa baadhi ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam
juzi, rais alisema ni kukosa adabu kwa baadhi ya Watanzania kuwatukana,
kuwadhihaki na kuwakejeli waanzilishi wa Tanzania, hayati Julius Nyerere na
hayati Abeid Aman Karume.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge),
William Lukuvi, amekiri kutoa maneno yanayodaiwa kuwa ya uchochezi kanisani kwa
madai ya kuingiwa hofu na harakati za asasi ya kidini ya Uamsho, kufanana na za
Chama cha Wananchi (CUF) za kudai Serikali ya mkataba.
Wajumbe wa Bunge Maalumu, wanaounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (UKAWA), wamesema hawatarudi bungeni na badala yake kuanzia kesho
wataanza mikutano ya hadhara nchi nzima kuwaeleza wananchi juu ya hila za Chama
Cha Mapinduzi (CCM) na washirika wake kutaka kuhodhi mchakato wa uandikaji wa
Katiba mpya.
Baada ya vuta ni kuvute sasa Wawakilishi wa Marekani, Muungano
wa Ulaya,pamoja na mawaziri wa kigeni wa Ukraine na Urusi wameafikiana kuwa
makundi yote ya kijeshi yaliyoko Ukraine bila idhini, yanafaakunyang'anywa
silaha na kuondoka mara moja kwenye majengo ya serikali wanayoyadhibiti
mashariki mwa Ukraine.
No comments:
Post a Comment