Wazazi wa Ramzan walisema walipinga uhusiano kati ya wawili hao.
Mwanamume aliyemuua kwa kumkata kichwa mpenzi wake amepatikana na hatia ya mauaji nchini Uingereza
Aras Hussein alimkata kichwa mwanafunzi mwenye
umri wa miaka 18 Reema Ramzan nyumbani kwake katika mtaa wa Sheffield
mwezi Juni kabla ya yeye mwenyewe kujidunga kisu kifuani mwake.
Aras amehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Hussein, alikiri kumuua mpenzi wake baada ya kuzozana ingawa awali alikana madai ya mauaji.
Mwili wa Ramzan ulipatikana katika sehemu ya jikoni ya nyumba ya Hussein tarehe nne mwezi Juni.
Polisi walipigiwa simu na mpita njia mmoja aliyemuona Hussein akitembea uchi nje akiwa na damu katika mwili wake.
Madaktari walipojaribu kumsaidia kwa kumpa
huduma ya dharura aliwauliza kwa nini walikuwa wanataka kumsaidia wakati
amemuua mtu nyumbani kwake.
Alipoulizwa kwa nini alifanya hivyo, akajibu kuwa hajui.
Mahakama ilisikia ambavyo msichana huyo alidungwa kisu kifuani na kisha kukatwa kichwa chake.
Pia mikono yake ilikuwa na alama za kuonyesha kuwa alijaribu kujikinga kutokana na kushambuliwa na mpenzi wake
Kiongozi wa mashitaka aliambia mahakama kuwa
marehemu Ramzan bado alikuwa hai wakati Aras alipoanza kumkata koo kwa
kutumia nguvu.
Wakati kesi ilipokuwa inaendelea , mahakama iliambiwa na familia ya Ramzan kuwa hawakupenda uhusiano kati ya wawili hao.
Siku ya kuuliwa kwake, alikuwa amekwenda nyumbani kwa Aras akiwa na Pasi yake ya usafiri pamoja na kitita kikubwa cha pesa.BBC
No comments:
Post a Comment