Pilika za maisha zimewafanya wachina wafikirie namna
wanavyoweza kuziba mapendo ya kushiriki katika shuguli za kijamii,ikiwemo
kuomboleza.
Miaka ya nyuma kiliwahi kutokea kikundi kama cha uombolezaji
nchini kilichokuwa na maskani yake maeneo ya mburahati ,Dar es salaam.Pengine
mahitaji ya soko wakati huo hayakukidhi gharama na utashi wao na hivyo
kusababisha kife.
Kwa kawaida maombolezo kwa mila na desturi za wachina hudumu
kwa siku 49 mpaka 100.kutokana na ongezeko la majukumu ,jamii hiyo imegundua
mtindo mpya ambao ni kukodisha watu wa kushiriki maombolezo .kwa pauni 300 za
kingereza (ambazo ni wastani wa sh 700,000),mtu anaweza kutumia kumlipa mwombolezaji
wa kukodi ili akachukue nafasi yake katika msiba.
Chen Shuqiang (35),kiongozi wa kikundi cha waombolezaji wa
kukodi katika mji wa Feishian ulikopo kusini Mashariki mwa China,anasema kwa
kiasi hicho cha pesa ambaco hulipwa kila mmoja,huufanya misiba ionekane kuwa
sehemu ya majonzi kwa kuwa huifanya kazi hiyo kwa uadilifu.
“kwa mila na desturi
za kichini mtu anapokufa hupata heshima zaidi iwapo watu watamlilia
sana,lakini ongezeko la majukumu limewafanya watu wengi washindwe kulitekeleza
hilo,hivyo sisi tukaona ni nafasi ya kujiajiri kusaidia hili “Shuqiang aliuambia
mtandao wa Daily mail.com.
Anaongeza kwa kusema kuwa siyo wafiwa tu ambao hawakukodisha
,kwani hata majirani ambao wanapaswa kushiriki misiba ,huwakodisha
wakawawakilishe.
“Mahitaji ya soko ni
makubwa kwani wanaohitaji huduma yetu siyo ndugu tu ,kwani hata majirani
wanaoalikwa huwalipa na kuwapa kadi zao za mialiko wakawawakilishe katika msiba
“anafafanua Shuqiang akikaririwa na dailymail.com
Anasema kazi yao kubwa huwa ni kulia na kujitupa huku na
kule karibu na jeneza.Huifanya kazi hiyo mpaka maiti itakapozikwa.
Chen Shuqiang akijitupa karibu na jeneza,pembeni waombolezaje wenzie
Mwanamke huyo anasema kabla ya kujiajiri kuwa mwombolezaji
,alikuwa akiimba katikakumbi mbalimbali lakini kazi hiyo haikuwa ikimlipa
vizuri.
“Tangu nimebadilisha ajira sijakutana na ugumu wa
kipato,hapa ninatafuta vijana wengine wa kuwaajiri kundini kwa kuwa soko
limekuwa kubwa na wanakikundi ni wachache “anasema shuqiang.
Desturi ya maombolezo
Mtu anapofariki,ndugu jamaa na majirani hutumiwa kadi za
mwaliko wa msiba.Kwa kawaida kadi hizi huwa nyeupe isipokuwa kama aliyekufa
alikuwa na umri wa miaka 80 au zaidi kadi huwa za rangi ya waridi.
Kwa umri wa miaka 80 kushuka chini,tukio hilo huwa msiba na
kama ni zaidi ya hapo.Huchukuliwa kuwa ni sherehe kwa kuwa mtu huyo ameishi
miaka mingi.
Dailmail.cominaeleza kuwa kadi hizo huandikwa wasifu wa
marehemu ,familia yake,tarehe ya kuzaliwa na kuzikwa .mazishi hufanyikakati ya
siku 49 lakini maombolezo huoendelea kwa siku 100 na zaidi.
Kama mwalikwa hatahudhuria mazishi,hukodisha watu lakini
hutakiwa kupeleka maua,shada na bahasha nyeupe yenye pesa ndani.
Waombolezaji huvaa nguo za rangi nyeupe.Wakati mwingine
wanaweza kuvaa nguo za rangi za rangi nyeusi na pinki iwapo aliyefariki ni mzee
wa miaka 80 au zaidi.MWANANCHI
No comments:
Post a Comment