Uchafuzi wa mazingira unasababisha maradhi ya mfumo wa hewa
,moyo na baadhi ya saratani lakini pia hivi karibuni wanasayansi wamebaini kuwa
uchafuzi wa mazingira ndicho chanzo cha wanawake kuzaa zaidi watoto wa kike kuliko
wanaume.
Watafiti hao waliangalia katika uzao wamiaka ya 2000 jijini Sao Paulo,na
mabadiliko ya kimazingira yanayotokea .Ilionekana kuwa ongezeko la uchafuzi wa
mazingira liliendana na ongezeko lakuzaliwa kwa watoto wa kike zaidi.
Kiongozi wa utafiti alibaini kuwa,uchafuzi wa mazingira una
madhara kwa mayai na mbegu za uzazi unaosababisha mimba za watoto wa kiume
zisitungwe.
Ilibainika kuwa kuna upungufu wa watoto wakiume
31,000 katika kipindi cha miaka saba iliyopita kulikotokana na uchafuzi wa
mazingira.MWANANCHI
No comments:
Post a Comment