Wanasayansi nchni China
wameuamsha ulimwengu kwa mara nyingine baada ya kubaini kuwa chai ndiyo
dawa kwa watu wanaotaka kuishi maisha marefu. Utafiti uliochapishwa
kwenye jarida la kimarekani la afya na maisha, ulieleza kuwa unywaji wa
chai unasaidia kwa asilimia 10 kupunguza hatari ya kifo.
Watafiti hao walionyesha kuwa kunywa chai mara kwa mara kunapunguza
msongo wa mawazo, tatizo ambalo husababisha watu wengi kupoteza
maisha.Hata hivyo utafiti huo ulionyesha katika siku za karibuni sababu
za vifo si hali mbaya ya kiuchumi pekee ama jinsia, umri au elimu bali
ni baadhi ya tabia ikiwemo kula matunda na chai ya rangi. (green tea).
No comments:
Post a Comment