Bamia inafahamika kwa wengi katika jamii kwa ladha yake nzuri inapotumika kama mboga katika baadhi ya milo.
Wapo wanaoitumia kama kiungo cha mboga na wengine huifanya mboga kamili.
Bamia ina majina lukuki, wengine huiita okra, kwa jina lisilo rasmi la Kiingereza huitwa, ‘lady finger’ au gumbo.
Bamia ina majina lukuki, wengine huiita okra, kwa jina lisilo rasmi la Kiingereza huitwa, ‘lady finger’ au gumbo.
Bamia ni miongoni mwa mboga za majani ambazo kwa kisayansi huitwa, ‘Abelmoschus Esculentus’
Kwa kawaida hulimwa zaidi kwenye maeneo yenye joto, ukanda wa kitropiki ikiwamo mikoa mikavu kama
Dodoma, Singida katika Tanzania.
Kwa kawaida huwa na rangi ya kijani iliyokolea na hukua hadi kuwa na urefu wa sentimeta tano hadi 15.
Zijue faida za bamia kiafya:
Bamia inaweza kukusaidia wewe ambaye umekuwa mtu wa kusahau mara kwa mara,na katika upishi wake usitumie viungo vingi tumia mafuta,kitunguu maji na nyanya pia chumvi kiasi kwa ajili yaladha na isiive hadi ikapoteza ukijani wake.Angalau ukawa unatumia kwa wiki mara mbili basi itakusaidia sana.
Bamia ina wingi wa vitamini A ambayo husaidia kutengeneza kinga ya sumu. Kwa kifupi, sumu inapoingia mwilini bamia huzuia kusambaa kwake.
Hata hivyo Bamia ina Vitamini A ambayo husaidia kuupa mwili wako kinga ya kupigana na maradhi.Kwa wenye matatizo ya kuona, kula bamia mara kwa mara pia kutaimairisha mwanga katika macho yako.
Wingi wa vitamini A huzuia maradhi yatokanayo na virusi kama mafua.
Uteute uliomo katika bamia husaidia kuunda tishu
za mwili na ngozi. Watu wenye ngozi laini na zinazoteleza wana kiwango
kikubwa cha ute ambacho husaidia kujenga ngozi.
No comments:
Post a Comment