Maria Sarungi ameomba mjadala kuhusu Hati ya
Muungano ufungwe hata kama itakayowasilishwa bungeni haitakuwa halisi.Mjadala
huo uliubuka bungeni kuanzia kwenye kamati, baadhi ya wajumbe wakidai sahihi za
hayati Mwalimu Nyerere na aliyekuwa Katibu wa Bunge, Pius Msekwa zimegushiwa.
Shughuli ya uokoaji wa abiria
waliokuwa ndani ya Meli iliyozama jana Korea kusini imeingia siku yake ya pili
hii leo maafisa wakiendelea kutafuta takriban abiria 289 waliokuwa ndani ya Meli hiyo ambao kufikia sasa hawajulikani walipo.
Kiongozi wa jimbo lenye idadi
kubwa ya watu nchini Australia,New South Wales, amejiuzulu baada ya kukosa
kutangaza kuwa alipata zawadi ya mvinyo yenye thamani ya dola 2,800.Waziri mkuu
wa New South Wales ,Barry O'Farrell alikiri kuwa alisahau au alighafilika kwa
bahati mbaya baada ya kuambia jopo moja linalochunguza visa vya ufisadi kuwa
hakuwahi kupokea mvinyo wowote kutoka kwa mtu yeyote.
No comments:
Post a Comment