Pages

Wednesday, March 19, 2014

JAMANI WATANZANIA TUMSAIDIE NOORAH




Mwanamziki Noorah amewaomba watanzani na wasanii wenzake kuweza  kumchangia ili aweze kulipa deni la matibabu,analodaiwa baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo Februari 20 mwaka huu.

Noorah alifanyiwaupasuaji baada ya kuanguka gafla na kugundulika kuwa utumbo wake ulikuwa umejisokota.Alilazwa hospital ya Kairuki iliyoko Mikocheni na kufanyiwa upasuaj.

“Ninadaiwa sh 2.7 milioni.hili debi ni baada ya kufanyiwa upasuaji “alisema mwanamziki huyo na kuwaomba watanzania kumchangia kwa hali na mali,huku wakiweka utaratibu wakuangalia afya zao mara kwa mara.


“Jamii iweke utaratibu wa kupima afya mara kwa mara ili waweze kujua magonjwa nyemelezi.mimi nimekuwa nahuu ugonjwa kwa miaka 20 niliumwa sana tumbo,lakini sikujua kuwa utumbo ulikuwa ukijisokota.kama ningekuwa na utaratibu wa kupima afya ningelijua mapematatizo.
 

No comments:

Post a Comment