Rapa K'Naan
Huku uvumi kuhusu masuala ya mahusiano ya kimapenzi ukizidi
kuenea kuhusu mshindi wa tuzo za Oscar mkenya Lupita Nyong’o kuna habari
moja inaendelea kung’ang’ania .
Lupita katika pozi
Lupita na rapa K’Naan wameonekana wakiwa pamoja na vyombo
vya habari vinaendelea kuikuza habari hiyo.Ripoti kuhusu maisha ya mapenzi ya Lupita ni dalili kuwa nguvu ya nyota huyo
inazidi kila kukicha.
Rapa huyo ni mzaliwa wa Somalia mwenye uraia wa Canada
amabaye ana umri wa miaka 36,aliyekulia Mogadishu,Kabla ya kuhamia Marekani na
baadaye Canada wakikimbia vita Somalia.
Alijipatia umaarufu baada ya kushiriki katika Tuzo za 2008
BET Hip hop Awards Cypher.Hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuonekana kwenye Televisheni
nchini Marekani maisha yake yalivutia
mashabiki wengi wa hip hop ambao walianza kumchukulia kwa umakini zaidi.
No comments:
Post a Comment