Mh.Zitto Kabwe ameonekana
Kufurahishwa na ufafanuzi wa Jaji Warioba na hata Kupelekea kuwashawishi
Wajumbe wenzake kwamba, hawana budi kujadili namna ya Kuuboresha zaidi muundo
huo wa Serikali tatu badala ya kujadili Serikali mbili ambazo yeye mwenyewe amekiri
kwamba hazitakuwa Suluhisho la Kero za muungano
************************
Jamaa za abiria wa China
waliokuwa kwenye ndege ya Malaysia iliyopotea,wametisha kususia chakula ikiwa
maafisa wa utawala wa Malaysia watakosa kutoa taarifa kamili kuhusu ndege hiyo.
Jamaa hao wameelezea kukerwa mno baada ya
mkutano na maafisa wa shirika la ndege hiyo mjini Beijing. Maafisa wa Malaysia
nao wanasema kuwa wanafanya kila wawezalo katika kuisaka ndege hiyo.
***********************
Hali ya wasiwasi imetanda eneo
la Crimea kufuatia kuuawa kwa afisa mmoja wa kijeshi kwa kupigwa risasi.Jeshi
la Ukraine lilisema kuwa afisa huyo aliuawa wakati watu wenye silaha waliokuwa
katika sare za kijeshi za Urusi
walipofyatulia risasi kituo kimoja cha
kijeshi cha Ukriane cha Kiev.Afisa huyo ameuawa masaa machache baada ya Waziri
wa Mashauri ya Kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov kumwonya
**********************
Mkuu wa idara ya kupokea
malalamishi ya umma, Bi Thuli Madonsela, hivi leo anatarajiwa kutoa ripoti ya
idara hiyo kuhusu uchunguzi wa iwapo Rais Jacob Zuma alihusika katika ufisadi
ambapo inadaiwa kuwa alitumia pesa za umma dola milioni ishirini kukarabati
boma lake la kifahari liililopo katika kijiji cha Nkandla alikozaliwa.
No comments:
Post a Comment