Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo, ametangaza kiama kwa watumishi wazee na kukaribisha vijana wenye elimu
kushika nyadhifa za juu katika wizara hiyo.Waziri huyo alisema elimu ya chini
kwa mtumishi wa wizara yake kuanzia mhudumu itakuwa shahada ya pili ili kwenda
na kasi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia duniani.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba, ametoa siri ya msimamo wa majeshi ya Tanzania
kuhusu muundo wa Muungano wa sasa.Jaji Warioba ametoa siri hiyo huku kukiwa na
vitisho kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanaotokana na
Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na viongozi waandamizi wa serikali kwamba
muundo wa Muungano wa serikali tatu ukipitishwa jeshi litachukua nchi.
Makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana
waliendelea na mashambulizi yao dhidi ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba, ambaye tume yake imependekeza muundo wa serikali
tatu katika rasimu ya Katiba mpya.
Watu wanne, wakiwemo maafisa wawili wa
polisi, wameuawa jana usiku mjini Nairobi baada ya gari walilolizuia kulipuka,
lilipokuwa likielekea katika kituo cha polisi katika eneo la Pangani, jijini
Nairobi. Kulipatikana bomu la pili katika gari hilo baada ya mlipuko huo na
wataalamu wa mabomu waliliharibu.Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu
kuitambua miili ya washukiwa hao.
Takriban watu 63 wamefariki
baada ya treni iliyokuwa imebeba abiria kupoteza mwelekeo Kusini Mashariki mwa
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.Msemaji wa serikali Lambert Mende alisema kuwa
polisi wanahofia kuwa idadi ya watu waliofariki huenda ikaongezeka. Pia alisema
kuwa polisi watafanya uchunguzi kubaini chanzo cha ajali.
No comments:
Post a Comment