Pages

Wednesday, April 23, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI



Mkazi wa kijiji cha Ng’ereng’ere Kataya Nyamaranga wilayani Tarime katika mkoa wa mara,Michael Bokoyo (60)anatuhumiwa kumuua binti yake mwenye umri wa miaka 10 kwa mpini wa jembe akimtuhumu kupalilia shamba vibaya.Mtoto aliyeuawa ni Neema Michael aliyekuwa mwanaunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Ng’ereng’ere kwa kumpiga na mpini wa jembe akimtuhumu kwa kuacha magugu shambani.

Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) inatarajiwa kupata ushindani baada ya Serikali kuamua kuruhusu wawekezaji wa sekta binafsi kutumia Reli ya Kati.Uamuzi huo wa Serikali huenda ukaongeza ufanisi kwa shirika hilo ambalo kwa miaka mingi limekuwa likikumbwa na matatizo ya kiufanisi

Kampuni ya Dongxing imeanzisha mradi wa ujenzi wa nyumba 98 utakaogharimu zaidi ya Dola 15 milioni kwa lengo la kuboresha maisha ya Watanzania.Akizungumza jana, Meneja Msaidizi wa Kampuni hiyo, Liu Yupeng alisema malengo ya mradi huo ni kuboresha maisha ya Watanzania na kuchangia katika ukuaji wa uchumi.

Kumezuka mapigano kati ya jeshi la polisi na wakaazi wenye hasira usiku kucha katika mojawapo ya viunga vya mji wa Rio de Janeiro. Barabara zimefungwa mjini humo wakati risasi zikisikika kutoka eneo hilo na polisi iking'ang'ana kuwadhibiti wakaazi hao.

.

No comments:

Post a Comment