Ikulu ya White House imesema kuwa imeshangazwa na
mauaji ya kinyama ya mamia ya raia Sudan Kusini na kutoa wito wa
kusitishwa kwa msururu wa vurugu zinazoendelea nchini humo.
Umoja wa mataifa ulisema siku ya Jumatatu kwamba
waasi waliwauwa mamia ya raia katika mji wa Bentiu na wengi walikufa
katika msikiti mmoja, hosipitali na kanisa ambako walikuwa wamekimbilia
kutafuta usalama.
Msemaji wa ikulu ya White House, Jay Carney,
amesema kuwa rais, Salva Kiir, na kiongozi wa waasi ni sharti watangaze
hadharani kuwa mashambulizi dhidi ya raia hayakubaliki.
Maelfu ya watu wamefariki dunia tangu mapigano ya kikabila yazuke mwezi Disemba mwaka uliopitaBBC.
No comments:
Post a Comment