Pages

Tuesday, April 22, 2014

MBUNGE MWINGINE AUAWA SOMALIA

Mbunge mwingine ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mogadishu, Somalia akiwa ni mbunge wa pili kuuawa mjini humo katika muda wa masaa 24.

Polisi wanasema kuwa Abdiaziz Isaq Mursal, aliuawa na watu waliokuwa wamejihami katika mkoa wa Medina.
 Mnamo siku ya Jumatatu, mbunge mwingine Isaq Mohamed Rino, aliuawa katika shambulizi la bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari,

Kundi la wanamgambo la Al Shabaab limekiri kufanya shambulizi hilo.
Serikali imeandaa kongamano la amani mjini Mogadishu kujadili nyenzo za kukabiliana na mashambuilizi ya mara kwa mara yanayoshuhudiwa nchini humo.

Mwezi jana, wanajeshi wa Muungano wa Afrika na wale wa serikali walianzisha operesheni mpya dhidi ya Al Shabaab.BBC

No comments:

Post a Comment