Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la
Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo, amekemea tabia ya utoaji
mimba inayofanywa na baadhi ya wanawake nchini kwani kufanya hivyo ni kupingana
na amri ya Mungu.Pia amekemea dhana potofu ya ndoa za jinsia moja kwa
kisingizio cha kukataa kupata watoto.
Wakati zikiwa zimesalia siku
nne kabla ya Bunge Maalumu la Katiba kuahirishwa, Mwenyekiti wa Bunge la Katiba
yuko visiwani Zanzibar kwa lengo la kuteta na viongozi wakuu visiwani humo.Ziara
hiyo ya Sitta ina lengo la kutoa taarifa za namna Bunge hilo linavyoendelea na
kupata mawazo ya namna bora ya kufikia lengo ambalo ni kupata Katiba mpya
Msemaji wa Ikulu ya White House
ametaja uchaguzi wa Urais uliopangwa kufanywa nchini Syria kama "Mzaha wa
Demokrasia".Jay Carney alisema matokeo ya uchaguzi huo hayatatambuliwa
nchini au nje.Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Ulaya wametoa maoni sawa na hayo,
na kusisitiza kuwa uchaguzi kama huo utavuruga utaratibu wa kisiasa nchini
humo.
Uchunguzi wa kina wa BBC
umethibitisha kuwa baadhi ya wakazi wa mpaka wa Niger na Nigeria wamekuwa
wakishirikiana na wapiganaji wa Boko Haram ili walipwe pesa.Nchi zilizo jirani
na Nigeria, kama Niger, Cameroon, na Chad zinahofia kuwa harakati za wanamgambo
hao zitaathiri usalama wa nchi hizo.
.
No comments:
Post a Comment