Uvumi ulioenea kuwa wanamuziki
mapacha Peter na Paul wanaounda kundi la P Square kutengana kwa kile
kinachodaiwa ni ugomvi mkubwa uliozuka baina yao,hauna ukweli wowote.
Mwishoni mwa wiki iliyopita
uvumi huo ulizagaa katika mitandao ya kijamii ukisema kabla ya kutengana
kulikuwa na ugomvi mkubwa uliowafanya wafikie hatua ya kupigana ngumi.
Msemaji wa kundi hilo la Nigeria,Bayo
Adetu alikanusha uvumi huo na kusema hajui aliyeandika habari hizo kazitoa
wapi.
“Ninajua kuna waandishi
wanatafuta umaarufu kwa nguvu.Sitaki kumpa nafasi hiyo huyu alieanzisha hiyo habari
ambayo haina ukweli wowote “alisema Adetu
Hata hivyo mtayarishaji na
mchambuzi wa Filamuwa Nigeria,Chris Novia aliuambia mtandao wa nolywoodnews kuwa walioanzisha habari
hizo ni P Square wenyewe na lengo lao ni kuongeza mauzo ya albamu yao.
“Huu ni uongo uliotungwa na P Square
wenyewe kwa sababu albamu yao ilikaribia kutoka .Hakuna kingine zaidi ya kutaka
kuongeza mauzo.alisema Adetu
No comments:
Post a Comment