Watafiti wamegundua kuwa juice ya nyanya inauwezo wakutibu
saratani na pia ni kinga na tiba ya maradhi mengi, hivyo ndugu yangu hutakiwi
kudharau ,Usimenye maganda,usiweke chumvi au sukari wala usichuje.
Nyanya (tomatoes) hutoa kinga mwilini dhidi ya ugonjwa wa
kiharusi au kupooza kama unavyojulikana na wengine.
Nchini Finland walifanya utafiti wa kina na kutoa taarifa
kuhusu kirutubisho aina ya ‘lycopene’ kinachopatikana kwa wingi kwenye nyanya,
matikitimaji na pilipili. Wamesema katika taarifa yao kuwa watu zaidi ya
1,000 waliowafanyia utafiti wenye kiwango kingi cha ‘lycopene’ kwenye mfumo wa
damu zao, hawakuonesha dalili kabisa za kupatwa na kiharusi.
Aidha, Chama cha Taifa cha wenye Kiharusi cha nchini
Marekani (The National Stroke Association) kimesema kuwa wanawake wengi
hufariki dunia nchini humo kutokana na kiharusi kwa idadi sawa na wale
wanaofariki kutokana na ugonjwa wa saratani ya matiti. Hii ina maana kwamba
ugonjwa wa kiharusi nao ni tishio kama ilivyo kwa ugonjwa wa saratani ya matiti.
No comments:
Post a Comment