Makombora ya maneno yaliyokuwa yakitolewa na
msemaji wa taarifa ya wachache bungeni, Tundu Lissu, juu ya muundo wa muungano,
na kutokuwapo kwa Hati za Muungano kumetikisa serikali ambayo sasa imeamua
kuzitoa hadharani hati hizo.
Uharibifu wa barabara uliotokana na mvua
zinazoendelea kunyesha, umeendelea kuwatesa wakazi wa Dar es Salaam na mikoa
mbalimbali nchini hasa baada ya mabasi ya mikoani kuzuiwa kufanya safari zake
jana.
Rais wa Urusi Vladimir Putin na rais wa
Marekani Barack Obama wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu .Masuala mbali
mbali kuhusu mzozo wa Ukraine, hususan upinzani wa wanaharakati wa kusini
mashariki mwa taifahilo dhidi ya sera za serikali ya sasa ya Kiev yamejadiliwa
baina ya viongozi hao.
Nchini Pakistan Polisi wamewakamata
wanaume wawili kwa makosa ya kuiba maiti ya mtoto kutoka kaburini na kisha
kumla.Wawili hao Arif Ali na kakake Mohammed Farman Ali waliachiwa huru baada
ya kuwa jela kwa miaka miwili kwa kula nyama ya binadamu.
No comments:
Post a Comment