Msemaji wa maoni ya wachache katika Kamati
namba 5, David Kafulila, amesema makada wa CCM hawana hadhi ya kumtusi
aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.Alisema
Warioba amefanya kazi kubwa katika taifa hili kuliko baadhi ya makada
wanaomdharau, kumtusi na kukebehi maoni ya tume aliyokuwa akiiongoza ambayo
ilipendekeza muundo wa serikali tatu unaokinzana na matakwa ya CCM inayotaka
serikali mbili.
Baadhi ya wenyeviti wa Kamati
za Bunge la Katiba wamezikataa taarifa za wajumbe walio wachache ambazo
wanapaswa kuzisoma leo bungeni, hivyo kuwataka waziandike upya kwa madai kuwa
hazijafuata taratibu katika uandishi na zimejaa lugha ya kuudhi.
Marekani imelaani kile
imekitaja kuwa hatua ya Urusi kutumia kaiwi kama chombo cha kuishurutisha
Ukraine.Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za Kigeni, Jen Psaki, amesema bei
ambayo Ukraine inalazimika kuilipa Russia kununua gesi haijaamuliwa na mahitaji
pamoja na kanuni za soko.
Baraza la Usalama la Umoja wa
mataifa limepiga kura kwa kauli moja kutuma kikosi kipya cha wanajeshi wa
kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati-kikosi hicho kitawajumuisha
wanajeshi karibu alfu kumi na mbili.Kwa sasa kuna wanajeshi alfu sita wa kikosi
cha umoja wa Afrika pamoja na alfu mbili kutoka Ufarnsa, lakini vikosi hivyo
vimekabiliwa na wakati mgumu kurejesha utulivu.
No comments:
Post a Comment