MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Herry Sameer ‘Mr Blue’,
amesema anatambua kuwa ana deni kubwa linalomuumiza kichwa analodaiwa na
mashabiki wake na yuko tayari kulilipa siku si nyingi.
Mkali huyo ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu tangu asambaze kazi
yake ya ‘Pesa’, ni kati ya wasanii wakongwe ambao wapo muda mrefu
kwenye ‘game’ na wanafanya vizuri.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Blue alisema, anajua kama
mashabiki wake wanamdai video ya wimbo huo, ambao umefanya vizuri
katika soko la muziki kutokana na ubora wa mashairi yaliyomo ndani
yake.
“Naamini ndani ya mwezi huu nitalipa deni kwa wapenzi wangu,
nimefanya kazi kwa Adam Juma na hivi sasa karibu namaliza, hivyo
mashabiki wakae mkao wa kula,” alisema.
Alisema, mbali na kutaka kuisambaza video ya ngoma hiyo, pia
anajiandaa kuisambaza kazi yake mpya inayojulikana kwa jina la
‘Clique’.
Blue alishawahi kutamba na vibao vyake kama ‘Johanita’, ‘Mapozi’ na
nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika vituo
mbalimbali vya redio.
No comments:
Post a Comment