Los Angeles, Marekani. Mwanamama mwenye ushawishi Duniani Opra
Winfrey, kupitia Kituo chake cha runinga cha ‘OWN’, amepata haki ya
kuonyesha filamu ya marehemu Mandela iitwayo ‘Long Walk to Freedom’.
Filamu hiyo imeshapata umaarufu mkubwa na kutajwa kuwania tuzo kadhaa. Itakuwa inaeleza maisha halisi ya mwanamapinduzi huyo.
Kwa mujibu wa waandaaji wa filamu hiyo, itachukua
miaka mitatu kabla ya kuanza kuonyeshwa kwenye runinga na itakapoanza
kituo cha kwanza kuionyesha kitakuwa ni ‘OWN’ ambacho kimenunua haki
hizo kutoka kwenye Kampuni ya ‘The Weinstein’.
Miongoni mwa watu waliowahi kumfanyia mahojiano yaliyojaa kila aina ya ushujaa, vilio hayati Nelson Mandela ni mtangazaji Opra ambaye alihudhuria mazishi ya mwanamapinduzi huyo jasiri Kijijini cha Qunu, alikozaliwa Mandela. From Mwananchi
No comments:
Post a Comment