Msanii wa filamu nchini Kajala Masanja amekanusha kuwa na uhusiano na wanaume na kusema anamsubiri mumewe ambaye yuko gerezani.
Kajala alianza kung'ara kupitia filamu ya Devil Kingdom aliyoshirikishwa na Steven Kanumba na muda mfupi baadaye alijikuta akiingia katika matatizokutokana na kushirikishwa kwenye uhalifu ambao unatuhumiwa kufanywa na mumewe.
Kajala anasema hana mpango wakuolewa na mwanaume mwingine kwa sasa .Alisema akiwa kama muumini wa dini ya Kikristo wa dhehebu la kanisa katoliki,hawezi kuolewa tena na kwa upande wake anaednelea kumsubiri mume wake.
Hata hivyo Kajala alitoa mwito kwa wasichana kuwa makini kabla ya kuingia katika ndoa.
"Mimi niliolewa kwa kuwa nilikuwa na matatizo yangu mwenyewe na ndiyo maana nikaamua kuolewa,lakini kumbe ndio nilijiingiza kwenye matatizo makubwa na kwa sasa naona kuwa ni bora ningetulia na kupenda kusoma.
No comments:
Post a Comment