Pages

Tuesday, April 08, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI





Watu wasiojulikana wamembaka na kumnyonga mkazi wa kijiji cha Mgango,kata ya Mgango wilayani Butiama mkoani Mara,Anastazia mang’ombe (42)wakati akiwa shambani kwake katika shuguli za kilimo.Kamanda wa polisi mkoani mara,Ferdinand Mtui alithibitisha kutokea kwa tukiohilo wiki iliyopita na kwamba hadi sasa jeshi hilo lina washikilia watu watatu kuhusiana na tukio hilo na kwamba upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Marekani imeelezea wasiwasi mkubwa kuhusu mzozo unaozidi kutokota mashariki mwa taifa la Ukraine ambapo makundi ya wanaharakati wanaoiunga mkono Urusi yameteka majengo ya serikali na kutangaza baadhi ya majimbo katika eneo hilo kuwa Jamhuri.Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani John Kerry ameionya Moscow kuwa kutakuwa na adhabu iwapo itaendelea na hila ya kuivuruga Ukraine.

Oscar Pistorius ameanza kujitetea katika kesi ya mauaji inayomkabili kwa kuiomba radhi familia ya Reeva Steenkamp.Kwa sauti ya kutetema, amesema alikuwa "akijaribu kumlinda" na amesema anashindwa kujua uchungu wanaoupata.

No comments:

Post a Comment