Mahakama moja nchini Misri imewahukumu watu wanne
kifungo cha hadi miaka minane jela kwa kosa la vitendo vya kufanya
mapenzi ya jinsia moja.
Watu hao wanashutumiwa kuhudhuria au kupanga tafrija za vitendo vya ngono, na kuvaa mavazi ya kike na kujipodoa.
Sheria ya Misri haitamki kupiga marufu vitendo vya mapenzi ya jinsia
moja, lakini waendesha mashitaka wametumia sheria ya Misri inayokataza
mambo fulani kufanyika hadharani kuwahukumu wapenzi wa jinsia moja.
Hukumu hiyo imeshutumiwa na wanaharakati wa haki za binadamu.
Mmoja wa watu hao amehukumiwa na mahakama mjini Cairo, kifungo cha miaka mitatu jela na kazi ngumu.
Kikundi cha kutetea haki za binadamu chenye
makao yake nchini Marekani, Human Rights First , kimesema hukumu hizo
zinasikitisha na kukatisha tamaa.
"Misri ni taifa linalobadilika katika eneo la
nchi za Kiarabu; kinachotokea Misri kinaweka hali ya kuenea katika
ulimwengu wote wa nchi za Kiarabu," kimesema kikundi hicho katika
taarifa yake.
Kikundi hicho kimesema tangu kung'olewa
madarakani Rais Mohammed Morsi mwezi Julai 2013
kumekuwa na ongezeko la
watu kukamatwa kwa misingi ya jinsia zao.
Hukumu ya sasa inakumbushia kesi ya mwaka 2001
ya watu 52 kushutumiwa kwa vitendo vya mapenzi ya jinsia moja na makosa
mengine chini ya sheria ya Misri.
Watu ishirini na watatu walihukumiwa kifungo cha
kufikia miaka mitano jela pamoja na kazi ngumu, hukumu ambayo
ilishutumiwa kimataifa.
Kikundi kimoja cha kutetea haki za binadamu
nchini Misri kimesema adhabu kali zilizotolewa kwa watu hao Jumatatu ni
sehemu ya msako unaoendelea dhidi ya uhuru binafsi.BBC
No comments:
Post a Comment